Tarehe 08 Machi, 2026 Balozi wa Tanzania nchini Japan aliandaa iftar kwa Diaspora wa Tanzania waishio Japan kufuatia mfungo wa Ramadhan unaoendelea.

Akiwakaribisha watanzania hao ubalozini kwa ajili ya kufuturu pamoja, alisema futari hiyo imeandaliwa kwa kutambua kuwa mwezi mtukufu wa Ramadhan ni mwezi wa toba kwa Waislamu hivyo tukio hilo lililenga kuwaleta pamoja waislamu na Wakristo ambao pia wapo katika mfungo wa Kwaresma.

Aidha, alitumia muda huo kuwataka waishi kwa amani kwa kuheshimu sheria za nchi mwenyeji na kuwaomba wajiandikishe katika Kitabu Maalumu cha orodha ya watanzania kwa lengo la kupata taarifa zitakazo rahisisha upatikanaji wao kwa ajili ya fursa na huduma mbalimbali watakapohitajika.