Tarehe 02 Febuari 2026 katika Ofisi za ubalozi Tokyo, Balozi Anderson Mutatembwa alipokea ujumbe wa Wataalamu 14 kutoka Tanzania waliowasili nchini Japan kwa ajili ya mafunzo ya muda mfupi ya kuwajengea uwezo katika masuala ya Gesi Asilia. Ujumbe huo unaongozwa na Bw. Nathan Mnyawami Mchumi Mwandamizi Wizara ya Nishati. Wengine ni Wataalamu kutoka Wizara hiyo, TPDC, EWURA na PURA walioambatana na Wataalamu kutoka JICA na Pacific Consultant Co. Ltd. Mafunzo hayo yanafanyika kwa awamu ya tatu kuanzia tarehe 02 - 13 Febuari 2026 chini ya Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) na kuratibiwa na kampuni ya Pacific Consultant Co. Ltd. Awamu zingine mbili zilifanyika mwaka 2025.




