📍YOKOHAMA, JAPAN

Tarehe 12 Mei 2024, Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda na watumishi wa @UbaloziJapan waliungana na wanadiplomasia wengine na umma wa Japan, katika matembezi na mbio za hisani, jijini Yokohama Japan.

Tukio hilo limeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (World Food Program- WFP).