TAARIFA KWA WATANZANIA WOTE WALIOKO NCHINI JAPAN

Ubalozi wa Tanzania, Tokyo unapenda kuwajulisha Watanzania wote walioko Japan kuwa Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda atakutana na kuzungumza na Watanzania wote waliopo Japan, tarehe 19 Machi 2023 kuanzia saa 4.00 asubuhi, kwenye Makazi ya Balozi (Tanzania House) jijini Tokyo. Aidha, pamoja na mambo mengine, siku hiyo utafanyika uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya wa Jumuiya ya Watanzania walioko Japan (Tanzanite Society) na kutakuwa na chakula cha mchana. 

Ubalozi unaomba ushirikiano wa Watanzania wote walioko sehemu mbalimbali za Japan kujitokeza kwa wingi katika siku hiyo. Tafadhali jiorodhesheni majina yenu kupitia Group la WhatsApp la Tanzanite au wasiliana moja kwa moja na Ubalozi kwa barua pepe tokyo@nje.go.tz au tzrepjp@tanzaniaembassy.or.jp  au/na namba ya simu 080 3441 1504/ 03 3425 4531 ili kurahisisha zoezi la maandalizi ya tukio hilo.

 

Imetolewa na;

UBALOZI WA TANZANIA - TOKYO