Ubalozi wa Tanzania Tokyo unapenda kuwaarifu wote kuwa, Ubalozi umeanza kupokea maombi ya Pasipoti za kielektonik kuanzia tarehe 21/10/2019. Muombaji atatakiwa kujaza fomu ya maombi kupitia tovuti ya Uhamiaji (www.immigration.go.tz) na kutuma maombi hayo ubalozini kwa email (passport@tanzaniaembassy.or.jp)
Jumla ya gharama ya maombi ya passport ni USD 90 ambazo zitalipwa kwa hatua mbili tofauti: -

 1. Hatua ya kwanza ni wakati wa kujaza fomu ambapo utalipia USD 15
 2. Baada ya hapo utazituma hizo fomu Ubalozini kwa njia ya email (passport@tanzaniaembassy.or.jp)
 3. Fomu zikipokelewa, zitafanyiwa kazi na utaletewa bili kwa ajili ya malipo ambayo yanaweza kufanyika online kupitia https://epay.gepg.go.tz au kwa benki za Tanzania. Malipo yote yatatumia control mumber iliyopo kwenye bili utakayoletewa.
 4. Hatua ya pili ya malipo ni baada ya kupata control number ambapo utalipa USD 75.
 5. Endapo malipo yatafanyika kupitia benki za nje (bank transfer) itachukuwa muda wa saa 24 kuhakiki malipo hayo.

Malipo yatakayofanyika kupitia benki za nyumbani Tanzania (Mfano CRDB) yatahakikiwa mara moja (ndani ya dakika 10).

 1. Baada ya malipo kuhakikiwa, muombaji atatumiwa stakabadhi yake.
 2. Muombaji atatakiwa kuomba miadi ya kuja Ubalozini kukamilisha hatua ya picha na alama za vidole. Kwa ajili ya picha vazi la juu (Shati au blauzi) inashauriwa kuwa rangi yoyote isipokuwa nyeupe na pink (inaweza kuwa rangi mchanganyiko) kutokana na kwamba background ya picha ni nyeupe.

Kabla ya kuja nitaomba chapisha (print) fomu zako na malizia kipengele cha 4 na 7.

Miadi hiyo itazingatia sana MUDA.

 1. Nyaraka zinazohitajika wakati wa kuomba pasi mpya za kielektroniki kwa Watanzania waishio Japan, Australia, New Zealand na Papua New Guinea
 • Hati ya sasa ya kusafiria (Current Passport)
 • Cheti chako cha kuzaliwa (Your birth certificate)
 • Hati ya kiapo au Cheti cha kuzaliwa cha mzazi mmojawapo ambae ni Mtanzania (Birth certificate or affidavit of one of your parents who is a Tanzanian)
 • Residence card (Gaijin Card) – Hati ya ukaazi
 • Kitambulisho cha Taifa kama kipo (National Identification card if any)
 • Barua ya kuomba passport (Covering letter)

Kwa watanzania waishio nje ya Japan na kwa sababu moja ama nyingine hawawezi kufika Ubalozini kwa ajili ya hatua za alama za vidole na picha, watalazimikia kwenda Tanzania au kusubiri upatikanaji wa Mobile equipment.

Tayari tumeshaomba Wizarani ila hatujaambiwa lini vifaa vitaletwa.

ANGALIZO
Ili kuepuka usumbufu, tunawaomba mfuate kwa makini maelekezo ya hapo juu hususan namba saba (Na. 7)